Kaloleni Pentekoste

KUHUSU SISI

DNPC - KALOLENI

Disciple Nations Pentecost Church (DNPC) Kaloleni ni kanisa lisilo la kimadhehebu linalopatikana Kaloleni Arusha, Tanzania. Kwa sasa tunakusanyika katika eneo hili, tukifanya kazi pamoja kusaidia jamii yetu kumjua Kristo. Ibada zetu zinakuwa mtandaoni moja kwa moja, karibu ujiungamanishe popote ulipo, sikiliza/tazama jumbe zitakazoleta mabadiliko katika maisha yako.

Tuna Amini katika

Mungu

Tunaamini kwamba Mungu mkamilifu alikuwepo, yupo na atakuwepo daima. Yeye ndiye Muumba wa yote tunayoyaona.

Roho Mtakatifu

Tunaamini kwamba Roho Mtakatifu ni uwakilishi wa tatu na wa mwisho wa Mungu. Anatuwezesha kwenye maisha na huduma.

Biblia

Tunaamini kwamba Biblia, vitabu vyote sitini na sita, vimevuviwa na Mungu. Inaelekeza imani na mazoea yetu.

Wokovu

Tunaamini kwamba mtu yeyote anaweza kupokea rehema kwa ajili ya makosa yake kwa kuweka imani yake kwa Yesu Kristo na kuyakabidhi maisha yake kwake. Sio suala la kazi; yote ni juu ya imani.

Njoo ujifunze neno la Mungu pamoja nasi

Tunaamini kwamba Yesu Kristo ndiye mwakilishi kamili wa Mungu: mwanadamu kamili na Mungu kamili. Hakufanya kosa wakati wa uhai Wake.